Jumapili, 9 Novemba 2014

USHINDI WA KWANZA MSIMBAZI

MICHEZO OKWI AIPA SIMBA USHINDI WA KWANZA
Hatimaye Klabu ya Simba ya DSM leo imevunja
MWIKO wa kutopata ushindi katika michezo ya Ligi
Kuu Tanzania bara msimu wa 2014/15 kwa kuitungua
Ruvu Shooting bao 1-0.
Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa
Dar es Salaam, haikuwa kazi rahisi kwa Simba
kupata ushindi, kwani licha ya kutawala sehemu
kubwa ya mchezo, imewachukua hadi Dakika ya 77
kupata bao hilo pekee lililotiwa kimiani na mganda
Emmanuel Okwi.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha Pointi 9 na
kupanda hadi nafasi ya 7 ikiwa imecheza mechi 7,
imefunga magoli 7, imefungwa magoli 6, Sare 6,
kushinda 1 na haijapoteza mchezo hata mmoja.
Mchezo unaofuata itacheza Desemba 26 katika
dimba la Taifa itakapoikaribisha Kagera Sugar.
Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, maafande wa
JKT Ruvu wameichapa Ndanda FC kutoka Mtwara
mabao 2-0.
JKT Ruvu imefikisha pointi 10, na kukwea hadi nafasi
ya 6 ikiiacha Ndanda FC katika nafasi ya 12 ikiwa na
point 6.
Baada ya michezo hiyo ya mzunguko wa 7, Ligi Kuu
itasimama hadi Desemba 26 mwaka huu.
Toa maoni yako kuhusu mwenendo wa Ligi ya msimu
huu.
39 mins · Public

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni