Matumaini ambayo wengi wetu tulikuwa nayo kumuona mshiriki wa kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa ya jumba hilo.
Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni